October 22, 2010

KUWEPO KWA NYARAKA BANDIA ZA KUPIGIA KURA

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Advocate Nyombi

 

Jeshi la
Polisi mkoani Mbeya, limemkamata na kumfikisha Mahakamani mfanya biashara mmoja ayelitoa taarifa za uongo kuwa katika eneo la Tunduma mpakani mwa Tanzania na Zambia kulikua na gari lililobeba nyaraka bandia na masanduku ya kupigia kura wakati huu wa kampeni na uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika(31 october) mwisho wa Mwezi huu nchini kote.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Advocate Nyombi,  kweli baada ya magari yaliyotajwa kufanyiwa upekuzi wa kina na kutopatikana kwa nyaraka na amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Victor Mateni(32), mkazi wa Sikanyihu Tunduma wilayani Mbozi.
Kamanda Nyombi amesema kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo, kumetokana na taarifa zake alizozitoa kwa Mkuu wa Idara ya Forodha mpakani hapo za kuwepo kwa nyalaka hizo kutokua zamasanduku hayo kama ilivyodaiwa na mtuhumiwa huyo.
Amesema “ Jumamanne Oktoba 19, mwaka huu mfanyabiashara huyo alimwendea Bw. Jovitas Kanisha Charles ambaye ni Mkuu wa Idara ya Forodha mpakani hapo na kumwambia kuwa gari lenye namba za usajili T.288 BHR aina ya Iveco likiwa na tela lenye namba T. 966 BKS mali ya Kampuni ya usafirishaji mizigo hapa nchini ya AZANIA lilikuwa limebeba shahasa na mabokisi hayo bandia na vilikuwa vikiingizwa nchini kwa siri”alisema kamanda nyombi.
Amesema Mkuu huyo wa Idara ya Forodha mpakani Tunduma, aliwasilisha taarifa hizo kwa Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama hapo mpakanai na kuitisha kikao cha dharura kuitathimini taarifa hiyo.
Kamanda Nyombi amesema wakati wa kikao hicho cha dharura kamati hiyo iliamua kufanya upekuzi wa kina katika gari hilo pamoja na tela lake ili kubaini ukweli wa taarifa hizo na kuchukua hatu za kiusalama.
Amesema wakati wa upekuzi huo, kamati hiyo pia ilimshirikisha mtoa taarifa ili naye ashuhudia kitakachopatikana lakini hadi mwisho wa upekuzi kulikuwa hakuna nyaraka ama masanduku ya kupigia kra yaliyobainika.
Amesema gari hilo lilikuwa na bidhaa mbalimbali za madukani ambazo ni za halali kwa kusafirishwa na kwa matumizi. Bidhaa hizo zilikuwa zikisafirishwa kutoka Afrika ya Kusini kwenda kwa wafanyabiashara wawili wa Jijini Dar es Salaam.
Kamanda huyo amesema baada ya upekuzi huo kutobaini kosa walimkamata mfanyabiashara huyo na kumfikisha makahakamani kwa kutoa taarifa za uongo na kesi yake imeahiirishwa hadi itakapotajwa tena Novemba 4, mwaka huu na mtuhumiwa amepelekwa rumande.
Huyo ni mtu wa pili kufikishwa mahakamani katika kipindi kisichozidi wiki moja kwa kutoa taarifa za uongo na kusababidha athari kwa watu wengine na taifa kwa ujumla.
Hata hivyo Kamanda Nyombi amesema makachero wa Polisi mkoani humo wanamsaka mtu mwingine ambaye pia alisaiidia kueneza taarifa za uvumi huo.
Jumanne wiki hii, Mwenyekiti wa Wazee wastaafu wa iliyokuwa Afrika ya Mashariki Nathanael Mlaki, alijisalimisha Polisi Jijini Dar es Salaam na kufikisha Mahakamani kwa madai ya kutoa taarifa za uongo kuwa mmoja ya wazee wastaafu wa iliyokuwa Jumuia hiyo amefariki dunia baada ya kumwagiwa maji ya kuwasha na Polisi wakati walipofunga barabara.

No comments:

Post a Comment