October 25, 2010

AHADI ZA WAGOMBEA UONGOZI WA NCHI, JE ZIPI ZINAZOTEKELEZEKA?


Ndugu zangu watanzania wakati zimebaki siku chache kupiga kura tumeyasikia mengi lakini leo tupime na kuangalia ni yapi yalioahidiwa na wagombea wa uraisi kutoka vyama mbalimbali vya siasa kama yatatekelezeka..... tumia haki yako ya msingi kumchagua kiongozi atakayekufaa..


AHADI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI KUPITIA MGOMBEA WAKE MHESHIMIWA DR. JAKAYA KIKWETE



Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
  1. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  2. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  3. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  4. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  5. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  6. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  7. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  15. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  20. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  21. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  23. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  24. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  28. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  30. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  31. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  32. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  35. Kulinda haki za walemavu- Makete
  36. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  37. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  41. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  42. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  50. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  53. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
  57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

NAYE MGOMBEA DR. WILBROAD SLAA KUPITIA CHADEMA


1.Kujenga nchi isiyo na ufisadi
2.Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
3.Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
4.Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
5.Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
6. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
7. Kutoa huduma bora za afya bure
8. kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
9. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
10. Kubana matuzi Ikulu (Yuko tayari kula mihogo

PROF. IBRAHIMU LIPUMBA WA CUF

1.Elimu ya bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu
2.Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri
3.Kuunda serikali shirikishi
4.Kusimamia rasilimali
5.Kuimarisha miundombinu
6. Kusimamia na kuboresha afya
7. Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji
8. Kurudisha chakula cha bure mahospitalini

kwa vyama vingine vya upinzani sera zao zinafanana kwa asilimia  kubwa . tucheki na upande wa zanzibar kwa Chama Cha Mapinduzi (Dr.Shein)na chama cha CUF  Sharrif Hamad


kwa upande wa Dr Shein kaahidi mengi kama..

1) Kuboresha maisha ya wavuvi-Chakechake Pemba
2) Kusomesha wafanyakazi-Mnazi mmoja
3) Kipaumbele katika elimu -Unguja na Pemba
4) Kipaumbele katika afya-Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba.
5) Kuulinda Muungano- Wawi kisiwani Pemba
6)Kuleta mabadiliko Zanzibar-Pemba na Unguja
7)Kuboresha Bandari ya Zanzibar kwa kuijenga upya-Kibandamaiti
8)Kuboresha Maendeleo Zanzibar- Jimbo la Wete, Pemba
9.Ujenzi wa maktaba kubwa na nzuri Kisiwani Pemba- Mtambwe
10.Kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu Zanzibar- Kijiji cha Kambini Mchangamdogo
11.Kuimarisha miundombinu Kisiwa cha Pemba- Kijiji cha Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba
12.Kuhamasisha wawekezaji kuwekeza Pemba katika miradi mbalimbali-Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba.
13.Ahadi eneo la Micheweni kuwa maeneo huru ya uchumi- Micheweni Kaskakzini Pemba
14. Kumaliza matatizo ya maji mkoani -Mkoani
15..Kujenga Bandari ya kisasa katika eneo la Mpiga Duri Unguja- Mkoani
16.Kuiamrisha makazi bora kwa Wazanzibar- Mkoani


na ndugu yetu wa CUF kaahidi haya..............

1. Zanzibar kuwa kama Hong Kong – Unguja
2.Kuendeleza mashamba ya Karume- Kibanda maiti
3. Kubadilisha katiba na kuunda katiba mpya ya muungano na Zanzibar- Pemba
4.Kubadilisha mfumo wa uteuzi makamishna wa tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC)- Unguja
5. Kuwaunganisha wazanzibari ili kujenga umoja, udugu na ushirikiano-Pemba
6. Kuwasilisha hoja ya kubadili katiba ya Zanzibar na ya Muungano-Viwanja vya Kibanda Maiti
7. Kuondoa bajeti ya ZEC isiwe chini ya waziri kiongozi na badala yake kuwa inajitegemea yenyewe- Pemba
8. Kuondoa ulazima wa mwenyekiti wa tume kuwa jaji na badala yake awe mtu anayejua sheria-Unguja
9. Serikali kuundwa na vyama vyote vilivyopata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi- Unguja
10.Kujenga jamii yenye maelewano na umoja -Pemba
11.Kutokochagua kiongozi kwa urafiki bali kwa uwajibikaji na uadilifu -Unguja na pemba
12.Kudhibiti vyombo vya dola vinavyofanya kazi kwa matakwa ya watu binafsi -Kibanda maiti
13.Kukomesha rushwa-Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba
14.Kuhakikisha ununuzi wa zabuni unakuwa wazi na wananchi kuruhusiwa kuhoji kuhusu zabuni-Jimbo la ole Pemba
15.Kuongeza kima cha chini cha mshahara hadi Sh150,000-Mkanyageni Pemba
16.Kubadili vikosi vyote vya usalama na kulipwa mishahara kima cha chini kulipwa Sh180,000-Chakechake Pemba
17.Kubadilisha kikosi cha KMKM kuwa kikosi cha mwambao-Wawi
18.Wazee kupanda daladala bure na wale wasiokuwa na watoto kulelewa bure-Majimbo ya Chakechake
19.Kufuta michango yote ya shule za msingi na sekondari, kila mwanafunzi kuwa na kompyuta na badala ya kuishia darasa la saba sasa kuishia kidato cha sita-Hoteli ya Bwawani
20.Kutoa kitambulisho cha kila Uzanzibari na kufuta cha Mzanzibari mkaazi- Uwanja wa Hospitali ya Mnazi Mmoja
21.Kila mzanzibar kupata pasi ya kusafiria- Hoteli ya bwawani Zanzibar
22.Kuanzisha shirika la ndege Zanzibar -Viwanja vya Kibanda maiti
23.Kupandisha uchumi wa Zanzibar kutoka 6.8 hadi 15 kila mwaka kwa Zanzibar -Unguja
24.Kutoa uhuru zaidi kwa vyombo vya habari pamoja na kusaidia uanzishwaji wa Baraza la Habari Zanzibar-Unguja na Pemba
25. Kuweka hadharani nambari yake ya simu - Viwanja vya Kibanda miti
26. Kubadili sheria ya uwekezwaji-Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar
27.Kila mwanafunzi kuwa na komputa yake-Viwanja vya Kibanda maiti
28.Akiwa rais hata waziri au mkewe atafungwa akiwa ametenda kosa-Viwanja vya Tibirizi Kisiwani Pemba
29.Kujenga bandari ya Mkokoto na Pemba ili kuweka usafiri wa haraka wa boti ziendazo kasi-Tibirizi Kisiwani Pemba
30. Ahadi kudhibiti kuvuja kwa mitihani- Unguja

No comments:

Post a Comment