October 21, 2010

ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA NA UJENZI WA TAIFA LILILO BORA LA BAADAE

nchi zinazoendelea zinaipa secta ya elimu kipaumbele lakini, tujiulize je hii elimu inayotolewa majengo yanaridhisha?. jionee moja ya jengo, ujiulize kwa staili hii kiwango cha elimu kinaridhisha kwa nchi kama Tanzania?

Waalimu nao hawasiti kuwaambia wanafunzi watafute sehemu yoyote watakayoweza kukaa ili wapate kufundishwa. tujiulize kwa namna hii wanafunzi wataweza kuyamudu masomo yao vyema?

Bila kuwasahau Waalimu, wote tunafahamu watu wa kuheshimiwa sana ni walimu kwani kupitia hawa walimu tunawapata Marahisi, Mawaziri,Wabunge, Maprofesa,Madokta na watu wengi sana walioelimika,  tujiulize maswali machache  hawa walimu wanathaminiwa? wanaishi katika mazingira yanayostahili? Wanapewa posho zao kwa wakati? wanaweza kujiajiri leo au kesho ambayo hawatakuwa katika kazi zao za kutegemea mwisho wa mwezi? Wanaweza kujenga nyumba zao wenyewe? ni hayo tu kuhusu walimu tena hawa ndio wanaostaili kuitwa WAHESHIMIWA!




Tunashangaa kuona hawa wanaojiita waheshimiwa wakiishi katika nyumba nzuri zenye thamani ya mabilioni bila hata kuwakumbuka hawa wenzetu waliosahaulika (walimu) waliowapa elimu, na hiyo elimu wakaitumia kwa manufaa yao wenyewe hii ni aibu na hata kujilimbikizia mali nyingi kama inavyo onyesha ktk picha hapo juu.

Kama sekta ya Elimu ingethaminiwa kama ilivyo sekta nyingine Serikali yetu ingekuwa wapi leo karne ya ishirini na moja? 

Watunga sheria wako wapi? Sheria zilizotungwa nazo zinafuatwa? sheria mnazotunga ni kwaajili ya akina nani?

1 comment:

  1. sina budi kumshukuru mmiliki wa blog ya lastepsodeofadit kwa ushikiano wake wa dhati alionipa katika kuwezesha blog yangu ya MTAZAMO kuwa hewani, mchango wake nauthamini sana na pia namuahidi 2takuwa pamoja katika kuuhabarisha umma mambo yaliyopo na pia hata yanayojiri. I give u big up m2 mzima pamoja 2naweza!

    ReplyDelete